Beki kisiki wa Yanga Lamine Moro amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya shilingi laki tano (500,000/-) kwa kosa la kumkanyaga mchezaji wa JKT Tanzania, Mwinyi Kazimoto ambaye naye amefungiwa mechi mbili kwa kosa la kusababisha vurugu kwenye mchezo wao uliopigwa Juni 17, 2020 kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma
Lamine alionyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo huo, tayari amekosa michezo miwili dhidi ya Azam Fc na Namungo Fc
Mchezo wa tatu ambao atakosa ni dhidi ya Ndanda Fc ambao utapigwa Jumamosi
Nyota huyo raia wa Ghana anaweza kurejea kikosini kwenye mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Kagera Sugar

ADVERTISE HERE