Mabao yake mawili yameinusuru Yanga kulala mbele ya Namungo Fc baada ya kufunga bao dakika za lala salama na kuisaidia Yanga kupata sare ya mabao 2-2
Ulikuwa ni mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Taifa jioni ya leo
Yanga itajilaumu yenyewe kwa kushindwa kuibuka na ushindi katika mchezo huo baada ya kukosa nafasi nyingi kwenye kipindi cha kwanza
Charles Manyama aliifungia Namungo Fc mabao mawili kwenye kipindi cha pili lakini kama sio Molinga leo pengine habari ingekuwa nyingine
Mwamba huyu kutoka DR Congo amekuwa akikosolewa sana na mashabiki wa Yanga, lakini kwa hakika wakati mwingine ameibuka kuwa msaada mkubwa kwa timu hiyo
Siku ya leo yeye anaweza kutajwa kuwa shujaa wa mchezo na pengine angekuwemo uwanjani tangu mapema, angeisaidia Yanga zaidi ya alichofanya dakika 30 alizocheza
Molinga amefikisha mabao 10 katika ligi kuu ya Vodacom