Huyu Morrison 'benchi' limuhusu Yanga

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
24 Jun 2020
Huyu Morrison 'benchi' limuhusu Yanga

Kitendo kilichofanywa na winga Bernard Morrison kutoroka kambini kisha kufanya mahojiano na chombo cha habari ni wazi hakikufanyika kwa bahati mbaya

Morrison amezungumza masuala yanayohusu mkataba wake kwa makusudi pengine kuipa Yanga hasira ili ivunje mkataba uliopo kisha  aweze kuondoka akiwa mchezaji huru

Kama Yanga imeweza kuthibitisha nyota huyo kuwa na mkataba wa miaka miwili, kwa nini aseme hana mkataba na Yanga?

Tena anazungumza hayo wakati timu ikiwa kambini kuelekea mchezo muhimu dhidi a Namungo Fc?

Hili ni jambo ambalo linaweza kuwavunja moyo wachezaji wanaojituma kuipambania timu kama watamuona nyota huyo akianzishwa kwenye kikosi cha kwanza

Yanga wamepita wachezaji wengi mahiri, na wengine kibao watakuja lakini hakuna mchezaji atakuwa mkubwa kuliko Yanga

Sasa kama mchezaji alisaini mkataba kwa hiari yake mwenyewe, kama anataka kuondoka si afuate utaratibu ulioainishwa na FIFA kwa timu zinazomtaka kuwasilisha ofa rasmi?

Uongozi wa klabu ya Yanga unapaswa kulivalia njuga sakata lake ili kukomesha baadhi ya timu ambazo zimekuwa na kawaida kuwahaa wachezaji

Msimu uliopita Yanga iliingia kwenye sintofahamu na mlinda lango Beno Kakolanya ambaye alitoroka kambini usiku wakati Yanga ikijiandaa na moja ya michezo ya ligi

Beno aliingia kwenye mtafaruko na aliyekuwa kocha wa Yanga wakati huo Mwinyi Zahera ambaye aligoma kumruhusu kurejea kikosini baada ya tukio lile

Miwisho wa siku Yanga ilivunja mkataba wake na akasajiliwa na Simba akiwa mchezaji huru licha ya kuwa mkataba wake ulikuwa mbioni kumalizika

Pengine na hili la Morrison linaweza kuwa katika mlolongo huo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
22h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’