Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema leo wanakabiliwa na mchezo mgumu wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa uwanja wa Taifa kuanzia saa moja jioni
Hata hivyo Eymael amesema baada ya kukosa ushindi katika mechi mbili zilizopita, wanahitaji kuondoka na alama zote tatu leo
"Mchezo wetu dhidi ya Namungo Fc hautakuwa mwepesi. Namungo wana timu nzuri, tulipocheza nao katika mchezo wa kwanza walitupa upinzani mkali. Kocha wa Namungo Fc nafahamiana nae vizuri, nimewahi kufanya nae kazi Rwanda. Nadhani utakuwa mchezo mzuri, mashabiki waje kwa wingi kushuhudia burudani," amesema
Nae kocha msaidizi wa mabingwa hao wa kihistoria Charles Mkwasa amesema wamefanyia kazi changamoto zilizowafanya wakose ushindi kwenye michezo iliyopita hivyo leo wana matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi
Kikosi cha Yanga kiliendelea kubaki kambini baada ya mchezo dhidi ya Azam Fc, kujiandaa na mcheo huo
Viingilio vya mchezo huo ambao utapigwa saa moja jioni, VIP ni Tsh 15,000/-, VIP B na C ni Tsh 10,000/- na Mzunguuko ni Tsh 5,000/-