Kaseke ataka akabidhiwe namba mbili 'mazimaa'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Jun 2020
Kaseke ataka akabidhiwe namba mbili 'mazimaa'

Baada ya kuonyesha kiwango bora katika nafasi ya beki wa kulia, nyota wa Yanga, Deus Kaseke, amesema kuwa haikuwa bahati mbaya kwake kucheza eneo hilo kwani analimudu vizuri na ikitokea katakiwa kuendelea kulitumikia, atalitendea haki.

Kaseke ambaye amekuwa akicheza nafasi ya winga wa kulia, juzi kwenye mechi ya Yanga dhidi ya Azam, kocha wake, Luc Eymael, alimtumia kama beki wa kulia nafasi ambayo huchezeshwa Juma Abduill.

Kaseke alipangwa kucheza eneo hilo baada ya Abdul kuwa nje ya uwanja akitumikia adhabu ya kadi tatu za njano alizozipata katika mechi zilizopita.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa suluhu, Kaseke alionekana kuimudu vizuri nafasi hiyo baada ya kutimiza majukumu yake ya msingi ya kukaba kiasi cha kutoonekana pengo la Abdul.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Kaseke alisema: “Sio kama ni bahati mbaya nimepangwa vile, bali ni nafasi yangu sahihi ninayocheza, lakini tangu nije Yanga, nimekuwa natumika zaidi winga wa kulia.

“Hata kama kocha akipendezwa kuendelea kunitumia katika eneo hilo, nipo tayari kwa sababu najua naweza kulimudu vizuri,” amesema

Kesho Jumatano Yanga inatarajiwa kushuka uwanja wa Taifa kuumana na Namungo Fc katika mchezo mwingine wa ligi kuu

Nahodha Msaidizi Juma Abdul amemaliza adhabu yake hivyo anatarajiwa kurejea kikosini na pengine Kaseke anaweza kurudishwa katika nafasi yake ya ushambuliaji kutokea pembeni, upande wa kulia

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’