Ulimwengu kurejea dimbani Januari, ishu ya kujiunga Yanga ni uzushi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
14 Nov 2017
Ulimwengu kurejea dimbani Januari, ishu ya kujiunga Yanga ni uzushi
Karibuni baadhi ya magazeti yaliripoti kuwa mshambuliaji wa zamani wa TP Mazembe Thomas Ulimwengu huenda akajiunga na Yanga kwa mkataba wa miezi sita ili kujiweka sawa zaidi kabla hajarejea nchini Sweden katika klabu yake ya AFC Eskilstuna.

Hata hivyo kulingana na taarifa aliyoitoa Ulimwengu mwenyewe ni kwamba jambo hilo halina ukweli wowote kwa kuwa kwa sasa hawezi kurejea dimbani mpaka mwezi Januari 2018.

“Namshukuru Mungu naendelea vizuri, nimeanza kufanya mazoezi ya uwanjani ya kwangu binafsi, kwani awali nilikuwa nafanya ya viungo tu,” amesema Ulimwengu.

“Hata hivyo sijajiunga na klabu yangu na sipo Sweden, kuna nchi nimejificha huku huku Ulaya najiweka sawa kwanza na daktari wangu ameniambia, nitarudi uwanjani kuanza kucheza Januari mwakani.”

Ulimwengu alifanyiwa upasuaji wa goti Julai 31 mwaka huu baada ya kuumia alipokuwa akiitumikia timu yake ya AFC Eskilstuna kwenye michezo ya maandalizi ya msimu mpya.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE →