Afisa Mhamasishaji na Msemaji wa klabu ya Yanga Antonio Nugaz amesema baada ya matokeo ya sare mchezo uliopita dhidi ya Azam Fc, hawatakuwa na huruma mchezo wa kesho dhidi ya Namungo Fc kwani wanazihitaji alama zote tatu
Nugaz amesema Yanga imejiwekea malengo ya kuhakikisha inamaliza msimu juu ya Azam Fc hivyo hakuna namna, kwa mechi zinazofuata watahitaji alama tatu tu
"Tunavyozihitaji pointi 3 za kesho dhidi ya Namungo Fc haijawahi kutokea, tunazihitaji sana kuliko kawaida kwa sababu zitatupa mwelekeo wa kukaa juu ya Azam," amesema
Aidha Yanga imewekea hadharani kuwa muda wa mchezo huo ni saa moja kamili jioni, viingilio vya mchezo huo vikiwa VIP A 15,000 , B&C 10,000 na mzunguko 5,000
Pia ukinunua jezi halisi Kwa bei ya ofa ya Shilingi 20,000 utapata jarida na tiketi ya mzunguko bure