Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe amesema vilabu vya Yanga na Simba vinapaswa kubaki mikononi mwa Wanachama, Wawekezaji hawapaswi kupewa hisa zaidi ya asilimia 49
Aidha, Dk Mwakyembe amevitaka vilabu hivyo kufanya tathmini ili kujua thamani yao halisi
"Nilitoa muongozo timu zote zilizoanzishwa na wananchi ziendelee kuwa mali ya wananchi na kama kuna wawekezaji basi wamiliki 49%. Kama wawekezaji wana misuli basi watengeneze timu zao"
"Lakini pia ni vyema vilabu hivi vikafanya tathmini ya kweli kufahamu thamani zao halisi. Nawapa changamoto kwa vilabu vyote hakikisheni mnafanya tathmini. Binafsi naona timu hizi zina thamani ya matrilioni na sio bilioni kama wanavyosema," alisema Dk Mwakyembe katika mahojiano na eFM mapema leo