Kessy akaribia kurejea Jangwani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Jun 2020
Kessy akaribia kurejea Jangwani

Beki wa kulia wa timu ya Taifa Hassan Kessy anaweza kurejea Jangwani baada ya kumaliza mkataba wake kunako klabu ya Nkana Fc, imefahamika

Kessy alitimkia Zambia misimu miwili iliyopita akitokea Yanga, ambayo pia aliitumikia kwa misimu miwili akitokea klabu ya Simba

Taarifa za uhakika ni kuwa yapo mazungumzo baina ya wakala wa mchezaji huyo na Yanga

Inafahamika kocha Luc Eymael alipendekeza kusajiliwa walinzi wawili wa pembeni upande wa kulia na kushoto

Tayari upande wa kushoto Yanga imefanikiwa kumnasa Mnyarwanda Erick Rutanga

Paulo Godfrey 'Boxer' ameonekana kutomshawishi Eymael ambaye jana kwenye mchezo dhidi ya Azam Fc alimtumia Deus Kaseke nafasi ya ulinzi upande wa kulia baada ya Juma Abdul kukosekana kutokana na kuwa na kadi tatu za njano

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
8h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
12h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
13h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
13h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’