Yanga iko tayari kuwasikiliza wanaomtaka Tshishimbi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
14 Nov 2017
Yanga iko tayari kuwasikiliza wanaomtaka Tshishimbi
Uongozi wa Yanga umesema upo tayari kuuza kiungo wake Papy Tshishimbi ingawa bado anamkataba hai wa miaka miwili.

Habari za uhakika kutoka kamati ya usajili wa Yanga zinasema kwamba mchezaji huyo anatakiwa nchini Afrika Kusini, Misri na Sweden.

Kaizer Chiefs, Mamelodi Sundowns za Afrika Kusini zinajipanga kuleta rasmi ofa mezani kwa Yanga pamoja na timu nyingine kutoka Misri ingawa Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa alikiri hakuna hata moja ambayo imeshakuja mezani hata wao wanasikia tu kutoka kwa wadau mbalimbali wa Jangwani ila amesisitiza utaratibu ufuatwe.

“Maombi yapo lakini katika hizo timu kutoka Misri na kwingineko hawajaleta barua kwamba kweli wanahitaji kumsajili Tshishimbi, lakini kama wakileta tutakaa nao chini na kuzungumza nao juu ya hilo,” alisema Mkwasa.

“Tshishimbi yupo katika mkataba na Yanga kama kuna timu yoyote kutoka hapa Tanzania au nje inamuhitaji kweli ilete barua ya maombi na sisi tutawambia pesa yetu ambayo tunahitaji ili kumsajili kiuhalali,” alisema Mkwasa bila kuweka rasmi makadirio ya dau wanalomuuza kwa madai kwamba mpaka iwe rasmi.

Mchezaji huyo amekuwa miongoni mwa vipenzi vya mashabiki kutokana na kiwango cha juu alichoonyesha hususani kwenye mechi mbili zilizopita za Simba na Yanga na michezo mingine ya ligi.

Dirisha la usajili linafunguliwa kesho Jumatano na litafungwa Desemba 15.

Kwa hisani ya Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →