FT : Yanga 0-0 Azam Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Jun 2020
FT : Yanga 0-0 Azam Fc

Mchezo wa ligi kuu ya Vodacom kati ya Yanga dhidi ya Azam Fc, umemalizika kwa timu hizo kugawana pointi baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana

Yanga iliyokuwa mwenyeji wa mchezo huo, iliuanza mchezo kwa kosa kosa za hapa na pale mapema lakini kukosekana kwa umakini katika safu ya ushambuliaji iliyoongozwa na David Molinga na Ditram Nchimbi, kuliinyima Yanga bao la mapema

Aidha, kwa nyakati tofauti mlinda lango Metacha Mnata aliokoa michomo mikali kutoka kwa washambuliaji wa Azam ambao walitengeneza nafasi za hatari zaidi

Kwenye kipindi cha pili kocha Luc Eymael alimuingia Bernard Morrison kuchukua nafasi ya Patrick Sibomana

Kuingia kwa Morrison kuliifanya Yanga iongeze kasi katika mashambulizi hata hivyo krosi nyingi alizokuwa akipiga ziliishia mikononi mwa mlinda lango wa Azam Fc

Yikpe Gnamien na Mrisho Ngasa nao wakaingia baadae lakini hawakubadili taswira ya mchezo

Matokeo hayo yanaibakisha Yanga katika nafasi ya tatu ikifikisha alama 56

Ni wazi Kwa Yanga, matumaini pakee ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao ni kwa kutwaa taji la FA

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’