Kessy awatahadharisha mashabiki wa Simba

Admin By Admin
•
1 Jul 2017
Kessy awatahadharisha mashabiki wa Simba
Tangu klabu ya Simba imrejeshe klabuni hapo mshambuliaji Emanuel Okwi kwa mara ya tatu, mashabiki wa timu hiyo wamekuwa wakitoa tambo za kila aina wakidai Yanga ijiandae kwa kipigo kuanzia mchezo wa Ngao ya Jamii utakaopigwa mwanzoni mwa mwezi Agosti.

Sasa mlinzi wa kulia wa Yanga Hassan Ramadhani Kessy amewaambia mashabiki wa timu hiyo watulie kwani siku hiyo watamkataa huyo Okwi.

Licha ya kukiri kuwa Okwi ni mchezaji mzuri lakini amewahakikishia mashabiki wa Simba kuwa hatakuwa na madhara yoyote timu hiyo itakapokutana na Yanga.

“Nimesikia majigambo wanayoyatoa Simba baada ya kumsainisha Okwi, niseme mimi sipendi kuongea, subirieni tutakapoonana uwanjani mimi nikiwa na Yanga na yeye Simba.

“Okwi siyo mchezaji mbaya, ni mzuri, ana uwezo mkubwa, lakini hatakiwi kupewa hizo sifa anazozipata kwa mashabiki wa timu hiyo.

“Kwa kifupi niseme kuwa tutaonana kwenye Ngao ya Jamii kabla ya kuanza ligi kuu halafu utaona kama wataongea tena,” alisema Kessy akiwa Afrika Kusini na timu ya taifa inayoshiriki michuano ya Cosafa.

Kessy ameimarisha kiwango chake na sasa ndiye chaguo la kwanza kwa kocha Lwandamina kwenye nafasi ya ulinzi wa kulia akimpiku rafiki yake Juma Abdul.

Kasi yake na uwezo wake wa kukaba ndivyo vinavyomfanya awe chaguo sahihi kwenye nafasi hiyo kwa sasa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE →