Kikosi cha Yanga kimeingia kambini leo kujiandaa na mchezo wa kigi kuu dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Jumapili kwenye uwanja wa Taifa
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wachezaji wote wako katika hali nzuri kueleka mchezo huo
"Tumerejea salama kutoka Dodoma, wachezaji wote wako katika hali nzuri na wanatarajia kuingia kambini leo"
"Tunashukuru hatuna majeruhi, Morrison tayari ameungana na wachezaji wengine, nahodha wetu Papy Tshishimbi leo atafanyiwa vipimo kubaini utayari wake kuelekea mchezo wa Azam," amesema
"Tunawaita mashabiki wetu waje kwa wingi kushuhudia burudani. Tunahitaji ushindi, sapoti yao itawapa hamasa wachezaji. Tulipoteza mchezo wa kwanza dhidi yao lakini hawajawahi kutufunga mara mbili hivyo mashabiki waje kwa wingi kushangilia ushindi"