Kiungo wa JKT Tanzania Mwinyi Kazimoto amesema amemsamehe beki Lamine Moro kufuatia tukio lililotokea baina ya wachezaji hao juzi kwenye mchezo wa ligi kuu
Kazimoto amesema Moro alimpigia simu kumuomba radhi hivyo kwa upande wake jambo hilo limemalizika

"Moro alinipigia simu baada ya mchezo, tulizungumza tukio lililotokea na kimsingi mimi nimemsamehe, nafahamu matukio kama haya hutokea kwenye soka," alisema kiungo huyo mkongwe
Mchezo kati ya JKT Tanzania dhidi ya Yanga ambao ulipigwa juzi kwenye uwanja wa Jamhuri, uligubikwa na matukio mengi ya kibabe yaliyopelekea wachezaji kushikana mashati mara kwa mara
Uongozi wa Yanga ulimchukulia hatua Moro kwa kumkata sehemu ya mshahara wake
Mwenyewe Moro ameeleza kujutia tukio hilo na ameahidi halitatokea tena