Keshokutwa Jumapili, kikosi cha mabingwa wa kihistoria Tanzania, Yanga kitashuka katika uwanja wa Taifa kuumana na Azam Fc ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Yanga iliyotokea mkoani Dodoma ilikolazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya JKT Tanzania, imejichimbia kambini kujiandaa na mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli ametaja viingilio vya mchezo huo , VIP ni Tsh 15,000/-, VIP B na C ni Tsh 10,000/- na upande wa mzunguuko ni Tsh 5,000/-
Mechi itapigwa kuanzia saa kumi jioni
ADVERTISE HERE