Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina amerejea mapema leo akitokea nchini Zambia alikohudhuria msiba wa mpwa.
Aidha kikosi cha Yanga kimerejea dimbani leo kuendelea na mazoezi katika uwanja wa uhuru baada ya mapumziko ya siku mbili.
Lwandamina amerejea na siri kubwa juu ya hatma ya washambuliaji Donald Ngoma na Amissi Tambwe kuelekea dirisha la usajili linalofunguliwa kesho Jumatano.
Kocha huyo raia wa Zambia ameiagiza kamati ya usajili ya Yanga inayoongozwa na Mwenyekiti Hussein Nyika kuhakikisha inasajili washambuliaji wawili matata.
Kati ya wawili hao imependekezwa mshambuliaji mmoja awe wa Kimataifa ambapo kwa hali hiyo italazimu kuvunja mkataba wa mmoja wa washambuliaji walio majeruhi.
Yanga itashuka dimbani Novemba 19 kuumana na Mbeya City kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 10.

ADVERTISE HERE