Winga wa Yanga Patrick Sibomana 'PS' anaweza kujihakikishia nafasi ya kuendelea kubaki na mabingwa hao wa kihistoria msimu ujao kutokana na kiwango chake kuendelea kuimarika
Bao alilofunga kwenye mchezo wa jana dhidi ya JKT Tanzania, limemfanya afikishe mabao sita na kushika nafasi ya pili nyuma ya David Molinga mwenye mabao nane
Yanga ikiwa inasubiri dirisha la usajili lifunguliwe ili ishushe majembe, Sibomana amejipambanua miongoni mwa nyota wa kigeni ambao wamekuwa wakitajwa kuwa katika mlango wa kutokea
Baada ya kurejea kikosini, Mkufunzi wa Yanga Luc Eymael amewapa changamoto wachezaji wake akiwataka watumie mechi zilizobaki kumpa sababu ya kuwajumuisha katika kikosi chake cha msimu ujao
Eymael amesema mpaka sasa ana majina ya wachezaji 10 ambao anaweza kuwasajili lakini idadi hiyo inaweza kupungua kama waliopo watamshawishi