Eymael ataja sababu ya kumpa nafasi Yikpe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Jun 2020
Eymael ataja sababu ya kumpa nafasi Yikpe

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema ataendelea kumpa nafasi mshambuliaji Yikpe Gnamien kwa kuwa hana machaguo bora zaidi ya washambuliaji kwenye kikosi chake

Mashabiki wa Yanga wameonyesha dhahiri kutomkubali mshambuliaji huyo aliyefunga mabao mawili, moja kwenye ligi na jingine kwenye michuano ya FA tangu aliposajiliwa mwezi Januari mwaka huu

Yikpe anaonekana kuwa chaguo namba mbili kwenye safu ya ushambuliaji baada ya Ditram nchimbi ambaye ni chaguo la kwanza

Mu Ivory Coast huyo anaonekana kuwapiku David Molinga na Tariq Seif ambao kwa mechi za karibuni wamekuwa na nafasi finyu kwenye kikosi cha kwanza

"Kwanza nataka mfahamu, sitaki kuzungumza mengi kuhusu Yikpe kwa kuwa sio mimi niliyemsajili, nilimkuta hapa"

"Lakini pia kwa sasa nalazimika kumtumia kwa sababu sina wachezaji zaidi kwenye safu ya ushambuliaji," alisema Eymael

Inaelezwa Yikpe amekuwa akifanya vizuri mazoezini na hivyo kuwashawashi benchi la ufundi lakini amekuwa hafanyi vizuri anapopewa nafasi kwenye mechi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’