Mapema leo, Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said alishiriki hafla ya uzinduzi wa Tawi la klabu ya Yanga Makao Makuu mkoani Dodoma
Akizungumza katika hafla hiyo, Hersi amesema Yanga inahitaji kusajili angalau Wanachama Milioni moja tu ambao watakuwa na uhakika wa kulipa ada ya kila mwaka ambayo ni Tsh 12,000/- (Tsh 1,000/- kwa mwezi)
"Kama wanachama milioni moja (1,000,000) watalipa ada ya uanachama klabu itaweza kupata Tsh. 12 bilioni kwa mwaka," alisema
"Gharama za kuiendesha klabu hazizidi Tsh. 4 bilioni kwa mwaka. Tutaweza kusajili wachezaji wenye hadhi na kulipa mishahara tarehe 20 ya kila mwezi, tutakuwa na uwezo wa kujenga uwanja wa mazoezi na kuboresha jengo la klabu na kuwa la kisasa"
"Tukiweza kuwa na Tsh. 12 bilioni kwa mwaka hatuhitaji mtu mmoja kwa ajili ya kuendesha klabu yetu, hatutaki mtu mmoja akinuna basi wanayanga wote tunanuna," alisema Hersi
Β Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, Yanga ina mashabiki zaidi ya Milioni 15, kinachotakiwa kufanyika ni kuwabadili mashabiki hao kuwa Wanachama ambao watachangia maendeleo ya klabu yao