Bosi mpya Yanga afunga mjadala wa Morrison

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Jun 2020
Bosi mpya Yanga afunga mjadala wa Morrison

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Wakili Msomi Simon Patrick amewatoa hofu wanachama na mashabiki wa timu kuwa winga Bernard Morrison ana mkataba na mabingwa hao wa kihistoria mpaka mwaka 2022

Aidha, Bosi huyo aliyeingia ofisini jana akichukua nafasi ya Dk David Ruhago ambaye mkataba wake ulisitishwa juzi, amesema nyota huyo ataungana na wachezaji wenzake siku ya kesho timu itakaporejea jijini Dar es salaam baada ya mchezo dhidi ya JKT Tanzania ambao unapigwa mkoani Dodoma leo

"Baada ya kuingia ofisini nilitaka kumaliza baadhi ya changangoto zilizopo na niliona nianze na hili la Morrison hivyo nilimuita ofisini, " alisema Patrick

"Nilizungumza nae kuhusu suala la kushindwa kusafiri na timu, nimebaini alipata majeraha siku mbili kabla ya timu kusafiri mkoani Shinyanga."

"Kosa alilofanya ni kushindwa kutoa taarifa sehemu husika, mwenyewe aliomba radhi na sisi kama klabu hatutamchukulia hatua zaidi. Ameahidi jambo hilo halitatokea tena"Β 

"Kuhusu hayo yanayoendelea huko nje, niwahakikishie Wanayanga kuwa Morrison ni mchezaji wa Yanga mpaka mwaka 2022, nazungumza hivi pia nikiwa Mwanasheria wa klabu," alisema Patrick

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’