Kiungo mshambuliaji wa Yanga Bernard Morrison leo alifika Makao Makuu ya klabu hiyo kuitikia wito wa Kaimu Katibu Mkuu Adv Simon Patrick ambaye ameanza rasmi majukumu yake mapya hii leo
Morrison hakusafiri na timu mkoani Shinyanga, lakini pia ni kuhusu alichozungumza hivi karibuni kuhusiana sakata la usajili na klabu ya Simba
Nyota huyo ameomba radhi na sasa atajiunga na kikosi cha Yanga baada ya mabingwa hao wa kihistoria kurejea kutoka Dodoma ambako kesho wanakabiliwa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania
ADVERTISE HERE