Wakati msimu ukielekea ukingoni, baadhi ya wachezaji wako katika presha kubwa, hofu ya nafasi zao kuchukuliwa na wachezaji wengine
Katika klabu ya Yanga, nyota wengi kwa sasa wanapambana kuhakikisha wanaendelea kubaki kwani wanajua, upo mkakati wa kuisuka upya timu hiyo
Mshambuliaji Yikpe Gnamien raia wa Ivory Coast ni miongoni mwa wachezaji ambao tetesi za kutemwa mwishoni mwa msimu zinamuandama
Hata hivyo Yikpe ameeleza kuwa na matumaini ya kuendelea kubaki na mabingwa hao wa kihistoria
Yikpe amesema atatumia mechi zilizobaki kuwaziba midomo wale wanaomkosoa
"Mechi bado zipo nyingi, nitahakikisha nafanya vizuri. Bado nina mkataba Yanga, hivyo sina wasiwasi nitaendelea kubaki hapa," alisema Yikpe ambaye yuko mkoani Dodoma na kikosi cha Yanga kinachojiandaa na mchezo dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa Jumatano
Katika mchezo dhidi ya Mwadui Fc uliopigwa mkoani Shinyanga, Yikpe alipoteza nafasi adimu ya kuifungia bao timu yake na pengine kurejesha imani ya mashabiki kwake