Eymael amkubali Yondani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Jun 2020
Eymael amkubali Yondani

Kocha Mkuu wa Yanga, Mbelgiji Luc Eymael, ameeleza kufurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na beki kisiki wa timu hiyo, Kelvin Yondani, katika mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui FC

Yondani, ambaye tangu kutua kwa Eymael amekuwa si chaguo lake katika kikosi cha kwanza, juzi alianzishwa akicheza kama kiungo mkabaji, namba sita dhidi ya Mwadui FC na kuonyesha uwezo mkubwa uliowasaidia kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Akimzungumzia beki huyo, Eymael alisema Yondani ameonyesha ubora wa hali ya juu kwa kucheza vizuri katika nafasi tofauti.

"Kelvin kacheza vizuri katika nafasi ya kiungo, kinachotakiwa kwake kwa sasa ni kubadilika na kuelekeza akili yake mchezoni, kaonyesha anaweza kuwa msaada kwa kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani," alisema Eymael.

Katika mechi hiyo ya kiporo cha Ligi Kuu iliyopigwa juzi katika Uwanja wa Kumkukumbu ya Kambarage mjini Shinyanga, bao hilo pekee la Yanga liliwekwa kimiani na Mapinduzi Balama dakika ya sita akiitendea haki pasi aliyorudishiwa na Deus Kaseke.

Yondani akisaidiana na mabeki wa kati, Lamine Moro na Juma Makapu, waliweza kuidhibiti vema safu ya ushambuliaji ya Mwadui FC ambayo ilionyesha uhai mkubwa dakika 15 za mwanzo za kipindi cha pili.

Yanga itashuka tena dimbani keshokutwa, Jumatano safari hii ikiwa ni katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kuwakabili JKT Tanzania na licha ya Eymael kuahidi kunaweza kuwa na mabadiliko kidogo katika kikosi chake, kwa sifa alizozitoa kwa Yondani ni wazi anaweza kumwanzisha tena.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’