Wakati uongozi wa Simba unakwenda kumshitaki Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela baada ya kutoa kauli kuwa wako kwenye mpango wa kumsajili kiungo wa timu hiyo Clatous Chama, baadhi ya wadau waliishauri Simba iachane na mpango huo kwa kuwa Mwakalebela mwenyewe aliomba radhi tena alibainisha kuwa hakumaanisha kile alichozungumza
Sasa ni kama mambo yamewageukia nao baada ya kiungo mshambuliaji Bernard Morrison kufichua mpango uliokuwa ukifanywa na timu hiyo kujaribu kumsajili kupitia njia za panya licha ya kuwa bado ana mkataba na Yanga
Uongozi wa klabu ya Yanga umedhamiria kulifikisha sakata hilo katika vyombo husika ili haki ikatendeke
Aidha, GSM kupitia Mkurugenzi wa Uwekezaji Mhandisi Hersi Said, wamesema jambo hili halitapita hivi hivi
"Sisi kama GSM pamoja na Yanga hatutafungia macho hili, tutalipeleka kwenye vyombo husika, na tunaamini kuwa TFF chini ya Rais Walace Kalia imekuwa ikitenda haki na katika hili watatenda haki. Sisi tunachofahamu Morison ni mchezaji wa Yanga Sc na ana mkataba mpka 14/7/2020, baada ya hapo tulimpa mkataba mwingine mpya wa miaka miwili," alisema Hersi
Kulikuwa na mpango wa kumkomoa
Kulingana na kauli aliyotoa Morrison mwenyewe, ni wazi Simba walifahamu kuwa nyota huyo raia wa Ghana amesaini mkataba kuendelea kucheza Yanga lakini bado waliendelea kumshinikiza asaini Simba kwa kuwa tayari walikuwa wamempa fedha dola elfu tano kama 'kishika uchumba'
Kama Morrison angesaini mkataba wa Simba ni wazi angefungiwa kuwa na pengine msimu ujao asingeweza kuonekana dimbani
Morrison hakusaini mkataba huo na pengine unaweza ukatumika kama ushahidi katika sakata hili