Kumekuwa na tetesi huko mtaani kuwa washambuliaji ambao wana mikataba iliyo hai na klabu ya Yanga Donald Ngoma na Amissi Tambwe kuwa huenda wakajiunga na Singida United.
Kocha wa timu hiyo Mholanzi, Hans van Der Pluijm, amezima tetesi kwa kusema hafikirii kuwasajili wachana nyavu hao.
Pluijm, kocha wa zamani wa Yanga ambaye ndiye aliyewasajili wachezaji hao kwa mara ya kwanza amesema hana mpango kabisa na wachezaji hao kwani anafahamu wana mikataba na Yanga.
Tetesi zimeenea kuwa huenda wachezaji hao wakatemwa ndani ya kikosi hicho kutokana na kuandamwa na majeraha.
"Hizo taarifa za kusema nataka kuwasajili Ngoma na Tambwe si kweli kwa sababu nafahamu wale wachezaji wapo kwenye mikataba na klabu yao hilo naliheshimu na sitaki kuliingilia," amefunguka Pluijm
"Zaidi napambana kuhakikisha naendelea kuijenga timu yangu kwa bidii hasa katika upande wa safu ya ushambuliaji ndiyo ninaifanyia kazi kwa kiasi kikubwa, masuala ya usajili kwa sasa siwezi kuyazungumzia," alisema Pluijm.

ADVERTISE HERE