Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael leo amemuanzisha mkongwe Kelvin Yondani katika nafasi ya kiungo mkabaji akianza eneo la kiungo pamoja na Mapinduzi Balama na Haruna Niyonzima
Aidha katika kikosi kinachoanza leo, Eymael amemuanzisha winga Patrick Sibomana 'PS' nafasi ya Bernard Morrison wakati Deus Kaseke akianza winga ya kulia
Ni kikosi chenye mabadiliko makubwa ukilinganisha na timu iliyocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC na kufungwa mabao 3-0 wiki iliyopita
ADVERTISE HERE