Yanga kamili kuikabili Mwadui Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Jun 2020
Yanga kamili kuikabili Mwadui Fc

Kikosi cha Yanga jioni ya leo kitashuka kwenye uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga kuikabili Mwadui Fc ukiwa ni mchezo wa kiporo, Ligi Kuu ya Vodacom

Baada ya kutokuwa na shughuli zozote za michezo kwa takribani miezi mitatu kutokana na ugonjwa wa corona, leo mikiki mikiki ya ligi kuu inarejea

Mchezo mwingine unaopigwa leo ni kati ya Coastal Union dhidi ya Namungo Fc

Yanga iliwasili Shinyanga tangu juzi na kuanza maandalizi yake jana ikipata nafasi ya kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Kambarage chini ya kocha wake mkuu Luc Eymael

Ni mchezo ambao Yanga inahitaji kushinda ili kurejesha imani ya mashabiki wake hasa baada ya kipigo cha mabao 3-0 kutoka wa KMC kwenye mchezo wa kirafiki

Pamoja na kuwa Yanga haina matumaini makubwa ya kutwaa ubingwa VPL, mechi za ligi zinaweza kuwa maandalizi mazuri kuelekea mechi za kombe la FA ambalo mabingwa hao wa kihistoria wanapaswa kulitwaa ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki mashindano ya Kimataifa msimu ujao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
11h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
14h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
19h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
23h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’