Tarimba afunguka kilichomkwamisha kufanya Mabadiliko Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Jun 2020
Tarimba afunguka kilichomkwamisha kufanya Mabadiliko Yanga

Wakati Yanga ikiwa imeanza safari ya kuelekea kwenye mabadiliko, Mkurugenzi wa Utawala wa Kampuni ya SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba, amesema aliwahi kushtakiwa kwa kiongozi mkuu wa nchi wakati akisimamia mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo

Mwenyekiti huyo wa zamani wa Yanga, amesema alikutana na upinzani kutoka katika kundi maarufu la Yanga Asili lililokuwa linapinga mabadiliko hayo ambalo liliongozwa na marehemu, Yusuph Mzimba.

Tarimba alisema hata hivyo hakukata tamaa na kila wakati aliendelea kuratibu mikutano mbalimbali ya kuelimisha wanachama na hatimaye sasa klabu hiyo imeamua kuanza upya mchakato huo.

"Mimi nilipelekwa hadi Ikulu kwa ajili ya kusimamia mabadiliko ya mfumo, nilikutana na ushindani mkubwa kutoka kwa baadhi ya wanachama ambao walikuwa wanauelewa tofauti, lakini kwa kushirikiana na wenzangu tulikuwa tunajaribu kutoa elimu ya kile tunachokitambulisha," Tarimba amenukuliwa na gezeti la Nipashe

Aidha, Tarimba amefunguka kuwa yeye ndiye mwanzilishi wa jina la Mnyama kwa sababu chini ya uongozi wake alipata mafanikio zaidi kila walipocheza na watani zao Simba.

"Katika kipindi changu nilipata mafanikio sana hasa dhidi ya Simba, sisi furaha yetu hata kama tumfunge nani, lakini kama hatukuweza kumfunga Simba, wala hakuna raha, usisikie masuala ya twende Afrika (Ligi ya Mabingwa Afrika), lakini heshima yetu ni kuifunga Simba, kwetu sisi Simba si maadui, ni marafiki zetu," alisema Tarimba.

Alisema siku Yanga ikitoka sare na Simba, hali huwa si shwari kuanzia barabarani hadi majumbani na aliongeza mpira bila ushindani, hakuna mpira.

"Simba si maadui ila ni washindani wetu, hebu angalia siku Yanga ikifungwa au ikitoka sare, hata majumbani hali inakuwa si shwari, mpira bila ushindani, hakuna mpira, hata nchi zilizoendelea utakuta kuna timu mahasimu, kama Manchester United ikicheza na Manchester City, si unajua panavyochimbika, hii inaleta ushindani kweli kweli," Tarimba alisema.

Alisema yeye haamini vitendo vya ushirikina na alipokuwa kiongozi wa Yanga alitoa ushirikiano kwa 'kamati za ufundi' ili kusaidia ushindi kwa sababu ni sehemu ya mila na tamaduni za Afrika.

"Miaka ya nyuma, enzi zetu zile, mabasi, watu wamebadilisha nguo zao na ukienda kwenye miti, bendera zimetanda, ile ilikuwa inaleta haiba kubwa kwenye mpira, wanaoroga ndio usiseme...lazima tuwe wakweli, sisi tuko Afrika, haya mambo yako kwenye asili, kweli si kweli, Mungu anajua," aliongeza kiongozi huyo.

Alisema pia alipokuwa kiongozi wa timu hiyo walikuwa wakijiridhisha na kikosi kinachopangwa kabla ya mchezo kulingana na uzito wa mechi husika.

"Kwa nia njema kabisa, wataalamu wa soka wanaweza waseme mwalimu asiingiliwe, lakini sisi kama viongozi timu inapofungwa, balaa liko kwetu, mwalimu anaenda kukaa hotelini, suala sio kutomwamini mwalimu, ni kujiridhisha," aliongeza Tarimba.

Hivi karibuni, uongozi wa Yanga kwa kushirikiana na wadhamini wao, Kampuni ya GSM, walisaini mkataba na LaLiga kwa ajili ya kuwasaidia mwongozo wa kuelekea kwenye mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’