Baada ya kuwasili mkoani Shinyanga mapema leo, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuanza maandalizi jioni kuelekea mchezo dhidi ya Mwadui Fc ambao utapigwa Jumamosi
Kiungo fundi wa timu hiyo Feisal Salum 'Fei Toto', ametamba kuwa wachezaji wote wana ari, wamefuata alama tatu huko Shinyanga
Leo Yanga itafanya mazoezi kwenye uwanja wa Fresho ulioko Shinyanga mjini

Aidha, baada ya kuwasili mkoani Shinyanga, wachezaji wote walifanyiwa vipimo vya corona ikiwa ni agizo la Serikali katika kuzingatia tahadhari ya maambukizi ya ugonjwa huo
Kesho Ijumaa, Yanga watapata nafasi ya kufanya mazoezi katika uwanja wa CCM Kambarage ambao utatumika siku ya Jumamosi
ADVERTISE HERE