Eymael ashangazwa wachezaji kuongezeka uzito Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Jun 2020
Eymael ashangazwa wachezaji kuongezeka uzito Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael ameeleza kushangazwa na taarifa za baadhi ya wachezaji wa timu hiyo kuongezeka uzito

Akizungumza na wanahabari jana baada ya kuwasili kutoka Ubelgiji, Eymael alisema, alikuwa akitoka program za mazoezi ambazo zingewasaidia wachezaji kubaki katika viwango vyao kabla ya corona

"Taarifa za wachezaji kuongezeka uzito nilizipata tangu nikiwa Ubelgiji. Inashangaza kwa sababu nilitoa program mbili za mazoezi ambayo kama wachezaji wangeyafanya kwa ufasaha wote miili yao ingekuwa sawa"

"Hii itakuwa changamoto kwetu kwani kwa bahati mbaya hata kocha wetu wa viungo (Berdien Riedoh) anaweza kuchelewa kurudi, mkewe atajifungua hivi karibuni," alisema Eymael

Agoma kuzungumzia ishu ya Molinga

Katika hatua nyingine, Eymael alieleza kupewa taarifa juu ya mshambuliaji David Molinga kugoma kusafiri na timu kwenda Shinyanga akidai 'kubainiwa' na kocha msaidizi Charles Mkwasa

Mbelgiji huyo amesema hafahamu nini kilitokea mazoezini kwani hakuwepo

"Nilitumiwa ujumbe na mtu nisiyemfahamu akinieleza kuwa Molinga analalamika kwamba kocha msaidizi hamtendei haki. Hata hivyo siwezi kuzungumza chochote juu ya hilo kwa kuwa sifahamu nini kilitokea kwenye mazoezi kwani sikuwepo," alisema

Eymael anatarajiwa kusafiri leo kwa ndege kuelekea jijini Mwanza kisha kuunganisha Shinyanga kuungana na kikosi cha Yanga ambacho keshokutwa kitashuka uwanja wa CCM Kambarage kuumana na Mwadui FC

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
14h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
18h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
23h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’