Molinga akacha safari ya Shinyanga, ajitetea

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Jun 2020
Molinga akacha safari ya Shinyanga, ajitetea

Mshambuliaji wa Yanga David Molinga amekacha safari ya mkoani Shinyanga kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwadui Fc ambao utapigwa uwanja wa CCM Kambarage siku ya Jumamosi

Molinga ni miongoni mwa wachezaji ambao walipaswa kuondoka Alfajiri ya leo, lakini Mcongomani huyo ameingia mitini kwa kile alichoeleza kuwa jina lake halikuwemo kwenye orodha iliyotangazwa na kocha Msaidizi Charles Mkwasa jana jioni

"Nataka nikanushe hii habari kwamba nimegoma kusafiri na timu. kwanza nimewakumbushe kitu cha peke imenileta Tanzania ni mpira na kazi yangu ndio iyo"

"Sasa iko ivi tangu timu imeanza mazoezi sijawahi kukosa na nafata program za Mwalim vizuri lakin jana list ilitoka na mimi jina langu ajakwepo sasa itasemekana vipi mimi nimegoma?"

"Kama ndio ivyo muulizeni coach ndio alitajia list yake. imekuwa tabia kila mara kila kitu mimi tu ata kama sijafanya kitu kibaya utaskia tu Molinga this is too much," aliandika Molinga kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

Hii sio mara ya kwanza kwa Molinga na Yanga kuingia kwenye mvutano hasa pale timu inaposafiri kwenda kucheza mikoani

Mchezo wa mwisho dhidi ya Namungo Fc kabla ya ligi kusimama kutokana na janga la corona, Molinga aligomea safari ya mkoani Lindi akitoa udhuru kuwa mkewe ni mgonjwa

Nyota huyo ameingia kwenye migogoro ya mara kwa mara na uongozi wa Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’