Kumekuwa na sintofahamu juu ya ujio wa kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael ambaye awali ilielezwa kuwa angefika juzi Juni 07 baada ya uongozi wa timu hiyo kufanikiwa kumkatia tiketi
Taarifa za uhakika ni kuwa Eymael ameondoka leo huko Ubelgiji ambapo atasafiri kwa zaidi ya masaa 24 akipitia Ujerumani, Ethiopia kisha kuuunganisha nchini
Safari ya Mbelgiji huyo imekuwa ndefu kwa kuwa bado baadhi ya nchi hazijarejesha huduma ya usafiri wa anga kutokana na changamoto ya ugonjwa wa corona ambao umeisimamisha dunia kwa karibu miezi mitatu
"Niko sawa, safari yangu ni Jumanne (leo), itanichukua muda mwingi mpaka kufika Tanzania, nitaondoka Ubelgiji mpaka Frankfurt (Ujerumani), huko nitaunganisha ndege nyingine mpaka Ethiopia ambako nitapata usafiri wa moja kwa moja Tanzania"
"Nadhani nitafika Tanzania siku ya Jumatano (kesho) saa saba na nusu mchana," alisema Eymael
Akitua nchini Eymael anaweza kuunganisha moja kwa moja mkoani Shinyanga kuwahi mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwadui Fc ambao utapigwa Jumamosi, Juni 13
Β