Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza kusitisha michezo yote ya kirafiki mpaka pale itakapojadiliana na timu za Yanga, Simba, Azam Fc, Transit Camp na KMC
Taarifa iliyotolewa na Shirikisho hilo usiku wa jana, ilibainisha kuwa hakuna mchezo wa kirafiki unaruhusiwa kuchezwa bila ya ruhusa yao
Hivi karibuni TFF ilivikumbusha vilabu vinavyoandaa michezo ya kirafiki kuzingatia tahadhari ya ugonjwa wa corona kama Serikli ilivyoelekeza
Hata hivyo kumekuwa na changamoto kuwadhibiti mashabiki ambao wanajitokeza kwa wingi kushuhudia michezo mbashara baada ya kukosa burudani hiyo kwa takribani miezi miwili

ADVERTISE HERE