Inaelezwa GSM wamemaliza kazi kwa winga wa AS Vita Tuisila Kisinda ambaye Wakala wake amethibitisha kuwa amepewa mkataba wa miaka miwili
Bila shaka usajili wa nyota huyo unasubiri wakati mwafaka utambulishwe kwani hata Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said, hivi karibuni alidokeza kuwa watamsajili winga huyo pamoja na mshambuliaji Mpiana Monzizi ambaye alikuwa akiitumikia Fc Lupopo
Mshambuliaji mwingine ambaye ametajwa kumalizana na kigogo huyo wa GSM ni Yacouba Sogne raia wa Burkina Faso ambaye alikuwa akicheza klabu ya Asante Kotoko ya Ghana
Kwa baadhi ya nchi ambazo zilimaliza ligi zao mapema, tayari michakato ya usajili imeanza kufanyika
ADVERTISE HERE