Yanga imepania kukisuka upya kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao mkakati namba moja ukiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ambao wameupoteza kwa msimu wa tatu sasa
Wakati akisubiriwa kutoa mapendekezo ya wachezaji ambao anahitaji kuendelea nao msimu ujao, Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael aliwapa changamoto wachezaji wake kumshawishi aweze kuwajumuisha
Mbelgiji huyo aliahidi kutumia mechi zilizobaki kwenye ligi ikiwa ni pamoja na mechi za kirafiki kuwapa nafasi baadhi ya wachezaji kudhihirisha ubora wao
Lakini kwa hakika ni kama wachezaji hao wanamrahisishia kazi Eymael kufanya maamuzi ya mwisho juu yao
Mechi hizi za lala salama ni muhimu kwa kila mchezaji kuonyesha ubora wake, na sio kinyume chake
GSM wamepania kuifanya Yanga iwe klabu bora, hasa wakati huu ambao timu imeingia kwenye mchakato wa mabadiliko
Wachezaji waliopo sasa walitakiwa kupambana kuonyesha wanahitaji kuwa sehemu ya 'project' hiyo
Lakini ni kama wanajikaanga wenyewe kwani baadhi yao wanakwenda kupoteza fursa adimu ambayo pengine ingewanufaisha katika maisha yao ya soka