Tumeyaona makosa, tutarekebisha - Mkwasa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Jun 2020
Tumeyaona makosa, tutarekebisha - Mkwasa

Kocha Msaidizi wa Yanga Charles Mkwasa amekiri vijana wake walizidiwa kimbinu na KMC hivyo kukubali kipigo cha mabao 3-0 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Uhuru

Mkwasa amesema vijana wake bado hawako fit, ukilinganisha na wapinzani wao KMC ambao wao walianza mazoezi mapema kuliko wao

"Ni kweli tumepoteza mchezo, ukiangalia ni makosa yetu sisi wenyewe yaliyopelekea tuadhibiwe. Mchezo huu umetusaidia kubaini mapungufu yetu na tutayafanyia kazi kabla ya ligi kurejea," amesema

"Niwapongeze wenzetu pamoja na kuwa wamefanya mazoezi kwa muda mrefu ukilinganisha na sisi ambao tumefanya mazoezi kwa wiki moja tu. Tunahitaji kuongeza nguvu pamoja na mazoezi mengine"

Yanga haikuwa na mchezo mzuri kabisa jana, safu ya ulinzi wakifanya makosa mengi huku safu ya ushambuliaji ikishindwa kufurukuta mbele ya walinzi wa KMC

Pengo la wachezaji Bernard Morrison, Papy Tshihimbi na Lamine Moro lilionekana dhahiri

Mkwasa aliwaweka nje Morrison na Moro ili kuwaepusha na majeraha zaidi kabla ya mchezo dhidi ya Mwadui Fc

Wachezaji hao walipata majeraha madogo kwenye mazoezi ya Yanga

Tshishimbi bado hajarejea uwanjani, anaendelea na matibabu ya jeraha la goti

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’