Yanga yamkomalia Sogne, kumpotezea Sarpong

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Jun 2020
Yanga yamkomalia Sogne, kumpotezea Sarpong

Wakati kukiwa na tetesi kuwa Yanga huenda ikamsajili kiungo wa zamani wa Simba James Kotei, taarifa zaidi zimebainisha kuwa mabingwa hao wa kihistoria wamemalizana na mshambuliaji wa Asante Kotoko Yacouba Sogne ambaye amemaliza mkataba na klabu hiyo

Sogne ni miongoni mwa wachezaji ambao walianza kufuatiliwa mapema na Yanga lakini dili lake lilikuwa gumu kukamilishwa kutokana na dau kubwa la usajili alilokuwa akitaka

Lakini kulingana na gazeti la Mwanaspoti, Wakala wa wachezaji Alfred Raul ambaye anaishi Ufaransa, amesema Meneja wa Sogne amemthibitishia kuwa nyota huyo anatua Yanga

Raul ambaye amedai kuzungumza na Yacouba pia, amesema nyota huyo anasubiri kuruhusiwa kwa safari za ndege huko kwao Burkina Faso ili aweze kuja nchini kusaini mkataba, akiwa tayari amesainishwa mkataba wa awali na mabingwa hao wa kihistoria

Dili la Yacouba huenda likafuta mpango wa Yanga kumsajili mshambuliaji wa Rayon Sports Michael Sarpong ambaye hivi karibuni klabu yake ilitangaza kumsamehe na kumrudisha kikosini

Aidha kuhusu ishu ya Kotei, Meneja huyohuyo wa Yacouba ndiye anayesimamia mpango wa kumleta Kotei ambaye kwa sasa anacheza kule nchini Belarus

Bernard Morrison na Lamine Moro ambao ni Waghana, wanatajwa kuwa na ushawishi kwa Kotei ambaye mwezi Januari aligoma kutua Yanga dakika za mwisho akidai atawaudhi mashabiki wa Simba

Ujio wa Kotei pia huenda ukafuta mpango wa Yanga kumsajili kiungo Ally Niyonzima ambaye anatajwa kuwa pendekezo la kocha Luc Eymael

Inaelezwa Yanga pia imekamilisha mazungumzo na aliyekuwa mfungaji bora wa ligi ya DR Congo Mpiana Monzizi wa FC Lupopo ambaye mpaka msimu unafutwa alikuwa na mabao 12 sawa na Jackson Muleka wa TP Mazembe

Pia mabingwa hao wa kihistoria watamshusha nchini winga hatari wa AS Vita Tuisila Kisinda

Usajili wa nyota hao juzi ulidokezwa na Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said ambaye ndiye anayesimamia dili zote za usajili zilizochini ya GSM

Injinia Hersi alidokeza kuwa watasajili mfungaji bora kutoka moja ya ligi tano bora barani Afrika lakini pia watamsajili winga hatari kutoka moja ya ligi hizo

Kulingana na takwimu zilizotolewa na shirikisho la soka barani Afrika (CAF) wiki iliyopita, Ligi ya DR Congo iko katika orodha ya ligi tano bora barani Afrika

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
7h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
11h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
12h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
12h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’