Mshambuliaji wa Yanga David Molinga ni miongoni mwa wachezaji ambao wamepewa program maalum baada ya kuongezeka uzito kipindi cha mapumziko ya corona
Nyota huyo huenda akakabiliwa na adhabu kwa kutofuata program za mazoezi zilizokuwa zikitolewa na benchi la ufundi baada ya kuongezeka kilo 12!
Aidha nyota wngine watatu; Yikpe Gnamien aliyeongezeka kilo 10, Patrick Sibomana (kilo saba) na Said Juma Makapu (kilo sita) nao wameingia katika mtego huo
Akizungumza na wanahabari kabla ya mazoezi jana jioni, kocha msaidizi wa Yanga, Charles Mkwasa alisema wachezaji hao wamepewa program ya mazoezi ambayo wanapaswa kuyafanya kwa wakati wao ili kuhakikisha wanarudisha uzito wao wa awali
"Baadhi ya wachezaji wawili/watatu wameongezeka uzito kidogo, tumewapa program maalum ya mazoezi ambayo wanayafanya kwa muda wao. Kwa ujumla wake mazoezi tumeanza vizuri, tunaendelea vizuri na vijana wanafanya kazi vizuri zaidi," alisema Mkwasa