Kocha Msaidizi wa Yanga Charles Mkwasa amesema kikosi chake kinafanya mazoezi kikamilifu tayari kuendelea na mechi za ligi kuu na kombe la FA
Akizungumza na Wanahabari kabla ya mazoezi ya leo jioni, Mkwasa alieleza kuridhishwa na muitikio wa wachezaji wake kwenye mazoezi
"Nina wachezaji 32, ambao kila siku wanakuja mazoezini. Wapo walioandikishwa na ambao hawakuandikishwa lakini nafurahi wote wanakuja mazoezi hakuna mchezaji anatega mazoezi," alisema
Aidha Mkwasa amebainisha kuwepo kwa baadhi ya wachezaji ambao waliongezeka uzito kipindi cha mapumziko ya corona, wamewapa program maalum
"Baadhi ya wachezaji wawili/watatu wameongezeka uzito kidogo, tumewapa program maalum ya mazoezi ambayo wanayafanya kwa muda wao. Kwa ujumla wake mazoezi tumeanza vizuri, tunaendelea vizuri na vijana wanafanya kazi vizuri zaidi"
Jumapili Yanga itacheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya KMC ambayo itapigwa kwenye uwanja wa Uhuru