Inaelezwa Yanga inaweza kumsajili kiungo wa zamani wa klabu ya Simba James Kotei ambaye hivi karibuni alitua nchini
Kotei kwa sasa anacheza soka la kulipwa huko Belarus barani Ulaya baada ya kuvunja mkataba wake na Kaizer Chiefs mwezi Januari
Yanga ilijaribu kumsajili nyota huyo mwezi Januari. Taarifa za uhakika ni kuwa mabingwa hao wa kihistoria wanaangalia uwezekano wa kumsajili nyota huyo hasa ikitokea wamemkosa kiungo mkabaji kiungo chaguo la kwanza Ali Niyonzima ambaye ni pendekezo la kocha Luc Eymael
Hata hivyo kama usajli wa Kotei utafanyika, huenda ukakumbana na upinzani mkali kutoka kwa baadhi ya mashabiki wa Yanga ambao hawakufurahishwa na kauli yake aliyotoa mwezi Januari kuwa kwa Tanzania hatacheza timu nyingine zaidi ya Simba akieleza kuwa na mapenzi na klabu hiyo
Baada ya Yanga kuanza mchakato wa mabadiliko ambao umewashuhudia wakiingia kwenye ushirikiano na La Liga na klabu ya Sevilla, inaelezwa wachezaji wengi wamevutiwa kujiunga na mabingwa hao wa kihistoria wakiamini hatua hiyo inaweza kuwa fursa kwao
Yanga itakuwa na nafasi ya kwenda kufanya maandalizi yake Hispania na itapata nafasi ya kucheza na vilabu vinavyosimamiwa na La Liga na hakuna shaka Sevilla pamoja na vilabu vingine ambavyo viko chini ya La Liga, vinaweza kuja nchini kucheza na Yanga
Lakini pia kulingana na mkataba wa klabu ya Sevilla, mchezaji mmoja mmoja wanaweza kupata nafasi kwenda kufanya majaribio katika klabu hiyo na pengine kusajiliwa katika academy zao na hata timu ya wakubwa