Tupo tayari, ushindi ni kila mechi - Abdul

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Jun 2020
Tupo tayari, ushindi ni kila mechi - Abdul

Nahodha Msaidizi wa Yanga Juma Abdul amesema wachezaji wa timu hiyo wana ari kubwa na wamepania kuwapa furaha mashabiki katika michezo iliyobaki

Yanga imerejea mazoezini wiki iliyopita, nyota hao wakiendelea kujifua chini ya kocha msaidizi Charles Boniface Mkwasa 'Master'

Abdul amesema wamepania kufanya vizuri katika michezo yote iliyobaki akitamba kuwa hawafikirii kama kuna mchezo watapoteza

"Wachezaji wako tayari, we mwenyewe si unaona namna tulivyo na ari kubwa katika mazoezi, tunajiandaa kikamilifu na michezo iliyobaki ya ligi na ile ya FA

"Hatutegemei kupoteza mchezo wowote tupo tayari kuikabili timu yoyote na tutapata matokeo chanya na sio kupoteza," amesema Abdul

Kipimo cha kwanza kwa mabingwa hao wa kihistoria ni siku ya Jumapili, Juni 07 ambapo wataumana na KMC katika mchezo wa kirafiki ambao utapigwa uwanja wa Uhuru

Baadae timu itaelekea mkoani Shinyanga ambapo Juni 13 itafungua rasmi ligi katika uwanja wa CCM Kambarage, kwa kuikabili Mwadui Fc

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’