Kikosi cha Yanga leo kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa shule ya Sheria, Mawasiliano, kujiandaa na mechi za ligi kuu ya Vodacom pamoja na kombe la FA
Kocha Msaidizi Charles Mkwasa ameendelea kuwanoa mabingwa hao wa kihistoria wakati wakimsubiri kocha mkuu Luc Eymael
Eymael amethibitisha kuwa ametumiwa tiketi ya ndege na uongozi wa Yanga hivyo atarejea nchini katika kipindi cha siku mbili au tatu
Jumapili, Juni 07 Yanga itajipima kwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya KMC





ADVERTISE HERE