Ni kama unaweza kusema suala la beki wa Coastal Union Bakari Nondo Mwamnyeto ambaye amekuwa akihusishwa na vilabu vya Yanga na Simba, limetamatishwa na kauli ya kibabe ya Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said ambaye amesema GSM haijawahi kushindwa katika jambo lolote walilosimamia
Mhandisi Hersi amesema kwa sasa nyota huyo bado ana mkataba na Coastal Union hivyo sio mali ya Yanga na sio mali ya Simba pia
Hata hivyo Hersi amesema ipo siku hatma yake itatambulishwa na vyombo vya habari
"Nikuhakikishie, hatujawahi kushindwa lakini kwa sasa Mwamnyeto si mchezaji wa Simba wala Yanga ila kuna siku utamtambulisha hapa," Mhandisi Hersi aliiambia Wasafi FM
Katika hatua nyingie Hersi amesema GSM haikuwahi kutaka kumsajili winga wa Simba Luis Miquissone kama ililivyoripotiwa na vyombo vya habari
Amesema dirisha la usajili litakapofunguliwa, watamshusha winga matata ambaye anatokea ligi bora barani Afrika
Amesema kocha Luc Eymael aliwaachia mapendekezo ya usajili ambayo kwenye kila namba alihitaji hadi wachezaji watatu