Mkurugenzi wa uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amesema mauzo ya jezi za klabu ya Yanga msimu huu yamevunja rekodi
Mapema leo akizungumza kwenye kipindi cha Michezo cha Redio Wasafi, Hersi amesema mapato ambayo Yanga wamepata kutokana na mauzoo ya jezi, hawajawahi kuyapata katika kipindi chochote huko nyuma
"Klabu ya Yanga imetengeneza pesa nyingi sana msimu huu katika mauzo ya jezi, haijawahi kupata Mapato kama hayo Hapo kabla.... .
Na kwa Tanzania Jezi ya Yanga Sc ndio imeuzika zaidi Tanzania"
"Mwaka huu tunaleta jezi yenye quality zaidi ya hiyo ili biashara iendelee kufanyika," alisema Hersi
Usajili kabambe wa ndani
Katika hatua nyngine, Injinia Hersi amesema wanasubiri uamuzi wa Serikali kuhusu mapendekezo ya idadi ya nyota wa kigeni wanaopaswa kusajiliwa na vilabu msimu ujao
Hata hivyo GSM wamejipanga kuboresha kikosi cha Yanga ambapo amebainisha kuwa mkakati uliopo ni kuwa watamsajili mchezaji yeyote wa ndani ambaye atakidhi vigezo vya kucheza Yanga
"Tutaheshimu uamuzi wowote utakaochukuliwa na Serikali kuhusu idadi ya nyota wa kigeni, hata hivyo tumejipanga, mchezaji yeyote wa ndani tutakaemtaka tutamsajili tukikosa tutaenda kuchukua nje ya nchi"