Mshambuliaji 'mwili jumba' raia wa Ivory Coast Yikpe Gnamien amerejea na moto mkali kwenye mazoezi ya klabu ya Yanga yanayoendelea Uwanja wa Chuo cha Sheria jijini Dar es Salam
Nyota huyo aliyetua Yanga usajili wa dirisha dogo, bado hajawashawishi mashabiki wa timu hiyo pamoja na kuwa tayari amefunga mabao mawili
Lakini mwamba huyo ameonekana kurejea na nguvu mpya akiwa anafanya vizuri kwenye mazoezi ya kikosi cha kocha Charles Mkwasa
Yikpe ameanza kuwafunika wenzie katika kutupia mabao mazoezini ikiwa ni dalili njema kwake
Kwa sasa ushindani unaonekana kuongezeka miongoni mwa washambuliaji wa Yanga, ni baada ya klabu hiyo kuweka hadharani mkakati wa kuiboresha safu yake ya ushambuliaji dirisha la usajili litakapofunguliwa
Kila mchezaji anapambana kuhakikisha anawashawishi mabosi wa Yanga na GSM ili aendelee kubaki kwenye kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria