Beki wa kushoto wa Polisi Tanzania Yassin Mustapha amewaita mezani mabosi wa Yanga waweze kumaliza nae ili ajiunge na timu hiyo
Mustafa amesema yuko ukiongoni mwa mkataba wake na Polisi Tanzania hivyo yuko tayari kujiunga na mabingwa hao wa kihistoria kama watafikia makubaliano
Nyota huyo alikuwa kwenye rada za Yanga tangu usajili wa dirisha dogo lakini makubaliano hayakufikiwa na timu yake ya Polisi Tanzania hivyo Yanga kuamua kumsajili Adeyum Saleh
"Mkataba wangu unamalizika mwishoni mwa msimu, niko tayari kujiunga na Yanga au klabu yoyote ambayo inanihitaji, ilimradi tu tukubaliane," alisema Yassin ambaye anatajwa kuwaniwa na Azam Fc pia
Yanga imeweka kipaumbele kumsajili beki wa kushoto wa Rayon Sports Erick Rutanga ikielezwa kuwa nyota huyo tayari amefikia makubaliano binafsi na wadhamini wa klabu hiyo, kampuni ya GSM
Hata hivyo wiki iliyopita klabu ya Polisi ya huko Rwanda ilimsainisha Rutaga mkataba wa awali na hivyo kuweka mashaka juu ya uwezekano wake wa kusajiliwa na Yanga
Lakini pia, taarifa nyingine zimedai kuwa kilichofanyia ni makubaliano binafsi ya Rutanga na Polisi kuwa ikitokea dili zake nyingine zimekwama, basi atajiunga na timu hiyo
Hivi karibuni kocha mkuu wa Yanga Luc Eymael alifichua kuwa Rutanga ni miongoni mwa wachezaji ambao anatamani kuwa nao kwenye kikosi chake msimu ujao