Niwapongeze kwa hili la leo, matamanio ya uendeshaji kwa Yanga ni ya muda mrefu toka kwa Castro Mponela alipokuja na Yanga kampuni , la pili alipokuwa Yusuf Manji alipokuja na dhana ya kukodisha hili litakuwa la tatu mengine yalikuwa kubadilisha katiba.
Mawili ya mwanzo hayakufanikiwa na yakaleta mgawanyiko kwa klabu. . La Castro lilizaa Yanga kampuni na Yanga asili. .mara nyingi alikuja kwangu kuomba msaada lakini mara zote nikwambia aje aelewane na wanachama wenzake.
Hata la Manji liliteta mpasuko kwa maana wengine waliridhia ukodishwaji na wengine kukataa. . kwa uelewa wangu changamoto hizi zilisababishwa na watu kutoelezwa na kueleweshwa vizuri pia hakukuwa na matayarisho ya kutosha.
Lakini awamu hii kwa hakika mchakato huu umefanyika kwa utaratibu mzuri hasa swala la kujifunza kutoka kwa watu wenye maarifa na uzoefu (La Liga)
Vizuri mna kamati inayojua matatizo yenu pia mna watu ambao wanauwezo wa kutatua matatizo yenu, kushirikiana na Sevilla sio jambo dogo, hii ni klabu kubwa na wametwaa ubingwa wa Europe League mwaka majuzi tu.
Mkiwa mnaenda na wanachama wenu matatizo yanapungua sana, ila ukiamini wewe ndo kiongozi na mna maamuzi ndipo mnatengeneza migogoro. . Niwapongeze sana kwa namna mnavyoenda nalo hili swala kwa hakika litakuja kuleta maendeleo makubwa. . Hata pale mnapokwama ni vema muombe msaada kwa wenye uwezo wa kutatua tatizo
Niwatakie kila heri, Daima Mbele Nyuma Mwisho