Yanga, La Liga, Sevilla kimeeleweka

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 May 2020
Yanga, La Liga, Sevilla kimeeleweka

Klabu ya Yanga imesaini makubaliano na kampuni ya La Liga ambayo itakuwa na jukumu la kushauri mfumo sahihi ya Uendeshaji wa klabu hiyo pamoja na kusaini mkataba wa ushirikiano na klabu ya Sevilla inayoshiriki ligi kuu ya Hispania

Mkataba wa ushirikiano baina ya pande zote umesainiwa usiku wa leo, ukianza kusainiwa kule Hispania na mabosi wa La Liga na Sevilla kisha kutumwa nchini kusainiwa na Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla kwa niaba ya Yanga na Mhandisi Hersi Said, Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM

Mkataba huo utaifanya Yanga kuwa klabu ya kwanza ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kuingia makubaliano ya ushirikiano wa moja kwa moja na La Liga

Aidha kupitia makubaliano hayo, Yanga itapata fursa ya kushirikiana moja kwa moja na klabu ya Sevilla katika ngazi zote kuanzia soka la vijana, kikosi cha kwanza na benchi la ufundi

Wachezji wa timu ya Yanga hasa vijana watapata fursa ya kwenda kufanya majaribio na kujiunga na timu ya vijana ya Sevilla huku viongozi na benchi la ufundi watapata fursa ya kwenda kujifunza Hispania

Tukio hilo la kihistoria lilishuhudiwa na Rais Mstaafu Awamu ya Nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alikuwa mgeni wa heshima

Aidha nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi na Juma Abdul wao waliwawakilisha wachezaji wengine katika tukio hilo lililoingia kwenye kumbukumbu za klabu ya Yanga

Sasa ni rasmi Yanga imeanza mchakato wa Mabadiliko chini ya ushauri wa La Liga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’