Leo saa 12 jioni pale Serena Hotel, Yanga inasaini mkataba na La Liga kwa ajili ya kusimamia mchakato wa Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa mabingwa hao wa kihistoria
Lakini pia, Yanga inakwenda kusaini mkataba wa ushirikiano na klabu ya Sevilla ambayo mwaka uliopita ililetwa hapa nchini ya kampuni ya SportPesa
Mkurugenzi wa Uwekezaji kampuni ya GSM Mhandisi Hersi Said amesema matukio hayo yanakwenda kufungua ukurasa mpya ambao utakuwa mwanzo wa mafanikio kwa klabu ya Yanga
"Jambo lolote lazima lianzie sehemu. Uendelezwaji wa fikra na maono ya kuijenga Yanga Mpya unachukua sura mpya leo," amesema
Tayari ukumbi umependeza kuelekea matukio hayo...!

ADVERTISE HERE