Bil 2.6 kutumika Mabadiliko Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 May 2020
Bil 2.6 kutumika Mabadiliko Yanga

Kwa mujibu wa Mkataba wa Yanga, GSM na Laliga utakaosainiwa wikiendi hii, pamoja na mambo mengine mabingwa hao wa kihistoria pamoja na wadhamini wao GSM, watailipa kampuni ya LALIGA Euro 1,040,000 (zaidi ya Bilioni 2.6)

Fedha hizo pamoja na gharama nyingine ndogo ndogo na kodi zitalipwa ili kugharamia mchakato wa mabadiliko ndani ya Yanga unaotarajiwa kukamilika Juni 30, 2023

Faida ambazo Yanga inakwenda kupata baada ya mchakato huo kukamilika

1. MFUMO WA KISASA WA KUENDESHA KLABU.

Klabu ya Yanga itanufaika kwa kupata mfumo bora na wa kisasa wa uendeshaji. Hii itagusa Idara zote za Yanga na zitakuwa na uwezo wa kujiendesha kisasa na kwa weledi. Laliga watashiriki kwa kiasi kikubwa kutoa mafunzo na utaalamu katika hilo.

2. UWAZI NA UWAJIBIKAJI

Klabu ya Yanga itanufaika kwa kuwa na mfumo wa uwazi na unao fuata misingi ya sheria na taratibu za uendeshaji ikiwa ni pamoja na uwajibikaji. Hii itaongeza Imani ya watu kwa Yanga Sc na kuwavutia wadau wengi wa ndani na nje ya Yanga Sc (Wawekezaji ) na kuifanya Yanga Sc kuwa klabu bora Afrika.

3. KUONGEZEKA THAMANI YA KLABU YA YANGA

Lengo kuu la mabadiliko haya ni kuifanya Yanga Sc kuwa klabu ya kisasa na kuongeza thamani yake katika soko la Uwekezaji. Kitendo cha kuwa na mfumo wa kisasa wenye uwazi na unao fuata sheria zote kutaivuta klabu ya Yanga Sc Karibu zaidi na makampuni ya ndani na kimataifa, Ushirikiano na kampuni kubwa ya LaLiga ni hatua moja ya kuelekea mageuzi ya klabu ya Yanga. Klabu Itakuwa na uwezo wa kuongeza thamani yake katika Uwekezaji maradufu

4. MAONO YA MUDA MREFU

Baada ya mfumo kukamilika klabu itakuwa na uwezo wa kupanga mipango yake kwa muda mrefu zaidi. Hii itainufaisha klabu hata kama kutakuwa na mabadiliko ya uongozi klabu kama taasisi itabaki imara na ikiwa na malengo yake ya muda mrefu.

Haya mambo tunayaona kwenye vilabu vya ulaya , mfano uchaguzi hauathiri malengo ya timu

5. UWEZO KIFEDHA

Baada ya mfumo kukamilika Yanga Itakuwa na uwezo mkubwa wa kujiendesha bila kutegemea udhamini pekee. Itakuwa na vyanzo vingi vya uhakika vitakavyo ongeza mapato ya klabu

6. BIASHARA & MAENDELEO YA MPIRA (Kibiashara Zaidi)

Maeneo ambayo yatanufaika ni pamoja na Masoko, Ushirikiano Kimataifa, Mauzo ya bidhaa za Klabu, Wadhamini , Utawala, Mapato ya Klabu, Mashabiki na Wanachama, Uendeshaji wa Mitandao ya Kijamii ya Klabu na mengineyo

7. YANGA YA KIMATAIFA

Klabu ya Yanga Itakuwa na fursa ya kuhudhuria matukio mbalimbali yaliyo chini ya LaLiga ikiwa ni pamoja na timu za vijanaΒ  zitapata fursa ya kwenda Hispania kushiriki mashindano maalumu pale inapotokea

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
14h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
18h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
19h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
19h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’